Watu 2,800 wamefariki kufuatia tetemeko la ardhi nchini Morocco

Dismas Otuke
1 Min Read

Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Morocco imefikia 2,800 huku matumaini ya kupata majeruhi yakididimia kila kuchao.

Takriban watoto laki moja wameathiriwa na tetemeko hilo la ardhi la mapema Jumamosi iliyopita kwa mujibu wa ripoti ya shirika la UNICEF huku watu wapatao 300,000 wakiathiriwa karibu na mji wa kitalii wa Marrakesh.

Shughuli za uokoaji zinaongozwa na mataifa washirika wa karibu wa Morocco ikiwemo Qatar, Uhispania, Umoja wa Milki za Kiarabu, UAE na Uingereza.

waokoaji wakifukua vifusi vya majengo nchini  Morocco

Matabibu wamekuwa mstari wa mbele kuokoa maisha ya majeruhi wanaotolewa kwenye vifusi.

Tetemeko hilo la ukubwa wa 6.8 kwenye kipimo cha Richter liliathiri miji kadhaa katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika ikiwemo Rabat, Marrakesh na Casablanca.

TAGGED:
Share This Article