Wa Iria na wengine saba kuhojiwa na EACC husu kashfa ya shilingi Milioni 140

Tom Mathinji
1 Min Read

Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Murang’a Mwangi wa Iria na watu wengine saba,  wanatarajiwa kufika mbele ya tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi EACC, kuhusiana na kashfa ya ufisadi ya takriban shilingi Milioni 140.

Kupitia kwa taarifa iliyotolewa jana Jumatatu, tume hiyo iliwataka wanane hao  kuhojiwa kuhusiana na ukiukaji wa sheria za ununuzi wa bidhaa za umma na pia utoaji wa zabuni za serikali ya kaunti ya Muranga.

“Tume hii inawawgiza watu hao kufika mbele yake katika makao makuu yaliyoko jumba la Integrity, au katika afisi yoyote ya EACC iliyo karibu Jumanne tarehe 16 Aprili bila kukosa,” ilisema taarifa hiyo.

Wa Iria atashtakiwa pamoja na Patrick Kagumu Mukuria, Jane Wanjiru Mbuthia, David Maina Kiama, David Mamma Njeri, Jane Waigwe Kimani, Solomon Mutura Kimani,na Peter Muturi Karanja.

Mnamo siku ya Jumamosi, Mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP, alisema wanane hao wanashtumiwa kwa kutoa zabuni na kujihusisha na makosa ya ununuzi wa bidhaa za umma za shilingi Milioni 140.

Mashtaka dhidi yao ni pamoja na kujihusisha na ufisadi,matumizi mabaya ya mamlaka,unyakuzi wa mali

Share This Article