Raia wa China ambao wanaishi na kufanya kazi nchini Tanzania wameanzisha ligi yao ya mpira wa miguu.
Ligi hiyo itakayohusisha timu 6 ilizinduliwa rasmi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge .
Alisema lengo kuu la ligi hiyo ambayo inadhaminiwa na benki ya “China Dasheng” ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Uchina.
Meya Songoro alisema pia kwamba ligi hiyo itatoa fursa kwa watanzania kujipatia riziki kupitia michezo.
Wasimamizi wa michezo hiyo ya soka ni raia wa Tanzania na wachezaji wa tanzania pia wamehusishwa kwenye baadhi ya timu.