Vyuo Vikuu vyatakiwa kushirikiana na sekta ya kibinafsi

Martin Mwanje
1 Min Read

Vyuo vikuu humu nchini vimetakiwa kubuni ushirikiano thabiti na sekta ya kibinafsi kwa lengo la kuuza ubunifu wao na kuratibu mipango ya masomo inayoambatana na soko la ajira.

Rais William Ruto amesema vyuo hivyo kadhalika vinapaswa kutoa masomo yanayonoa ujuzi wa wanafunzi na kutumia teknolojia kuimarisha upatikanaji wa shughuli za kimasomo.

Kiongozi wa nchi aliyazungumza hayo leo Jumatano alipotoa cheti cha kuhudumu kwa Chuo Kikuu cha Riara katika Ikulu ya Nairobi.

Aliongeza kuwa serikali imeongeza ufadhili kwa sekta ya elimu katika kipindi cha sasa cha matumizi ya fedha za serikali hadi shilingi bilioni 650 na kukariri dhamira ya serikali ya Kenya Kwanza kuimarisha upatikanaji wa fursa za elimu kwa Wakenya wote.

Chuo Kikuu cha Riara kilichopo katika eneo la Konza, kaunti ya Machakos kiliaanzishwa mwaka 2012 na wasomi tajika Daniel Gachukia na mkewe Prof. Eddah Gachukia,

Chuo hicho kimekuwa cha 69 kilicho na cheti kamili cha kuhudumu humu nchini kati ya vyuo 75 vinavyoendesha shughuli zao nchini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *