Vitambulisho 180,000 havijachukuliwa, asema Muturi

Dismas Otuke
0 Min Read

Waziri wa Utumishi wa Umma Justin Muturi amesema jumla ya vitambulisho 180,000 na leseni 47,000 havijachukuliwa na wenyewe kutoka vituo vya Huduma Centre kote nchini.

Pia vyeti 54,000 havijachukuliwa na wenyewe huku akiwataka wamiliki kuvichukua.

Waziri Muturi amefichua haya Jumatatu alipoongoza ufunguzi wa vituo 290 vya Huduma Centre katika kaunti ndogo  akianzia Tharaka Nithi, Kajiado, Kiambu na Laikipia.

Muturi aliongoza taifa kusherehekea wiki ya wateja kote duniani.

Share This Article