Vita vya zabuni vilichangia dosari za KCPE

Dismas Otuke
1 Min Read
Kiongozi wa Upinzani Raila odinga.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema Vita vya zabuni vilichangia dosari nyingi zilizoshuhudiwa katika mtihani  wa kitaifa wa darasa la nane KCPE  wa mwaka huu.

Raila anadai kuwa hatua ya serikali ya Kenya Kwanza kuipokonya kampuni ya Uingereza zabuni ya uchapishaji mtihani huo na kuipa kampuni ya Kenya yenye makao yake Mombasa Road ndio chanzo cha kasoro hizo.

Raila anadai kuwa serikali iliipokonya kampuni ya Uingereza zabuni kwa kukataa kuzunguka mbuyu.

Kampuni hiyo ya Mombasa Road pia ilitoa zabuni nyingine kwa kampuni ya India ili kuchapisha karatasi hizo kulingana na madai hayo ya Odinga.

Kulikuwa na dosari kataika matokeo ya mwaka huu baadhi ya wanafunzi wakipewa alama za masomo ambayo hawakutahiniwa.

Share This Article