Timu ya taifa ya Kenya ya soka Harambee Stars itashuka uwanjani Gombani leo Jumanne, kukabiliana na Kilimanjaro Stars ya Tanzania katika mechi ya pili kuwania Kombe la Mapinduzi kisiwani Zanzibar.
Mechi hiyo ni ya kufa kupona kwa pande zote baada ya Kenya kutoka sare ya bao 1 na Burkinafaso katika mchuano wa ufunguzi huku Tanzania ikizabwa bao moja kwa bila na wenyeji Zanzibar.
Harambee Stars watakamilisha ratiba Ijumaa hii dhidi ya Zanzibar.
Kenya na Tanzania zinatumia mashindano ya Mapinduzi Cup kunoa makali kwa fainali za nane za Kombe la CHAN mwezi ujao.