Visa vya ugonjwa wa Mpox nchini vyagonga 18

Martin Mwanje
1 Min Read

Idadi ya visa vya ugonjwa wa Mpox vilivyoripotiwa nchini imefikia 18. Hii ni baada ya kisa kingine kipya kuthibitishwa katika kaunti ya Nakuru. 

Kupitia kwa taarifa leo Jumatano, Waziri wa Afya Dkt. Deborah Barasa amesema hadi kufikia sasa, visa 4 vimeripotiwa katika kaunti ya Nakuru kufikia sasa, Kajiado (2), Taita Taveta (1), Busia (1), Nairobi (2), Mombasa (1), Makueni (1), Bungoma (2), Kericho (1), Uasin Gishu (1) na Kilifi (1).

Kulingana na waziri huyo, wagonjwa wanne walioambukizwa ugonjwa huo wanaendelea kupokea matibabu huku 14 wakithibitishwa kupona ugonjwa huo.

Dkt. Barasa amesema jumla ya wasafiri 1,900,967 wamepimwa ugonjwa huo katika maeneo mbalibali ya kuingia humu nchini tangu kuripotiwa kwa mlipuko huo nchini.

Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, wasafiri 14,311 wamepimwa.

Wizara ya Afya inasema inaendelea kuimarisha mifumo yake ya uangalizi wakati ikifuatilia mlipuko huo katika kanda hii.

Imewataka Wakenya kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Share This Article