Takriban visa 30,000 vya ugonjwa wa Mpox vimeripotiwa barani Afrika tangu kuzuka kwa ugonjwa huo, kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO).
WHO imesema kuwa vingi ya visa hivyo vimeripotiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na nchi jirani ya Burundi huku vifo zaidi ya 800 vikiripotiwa.
Kando na mataifa ya Afrika, visa vya Mpox vimeripotiwa katika mataifa ya Pakistan na Uswidi.
DRC inapanga kuanza kutoa chanjo kwa raia wake kuanzia tarehe 2 mwezi ujao.