Vipusa watatu wa Kenya wafuzu kwa nusu fainali ya mita 1500 Paris

Tom Mathinji
1 Min Read

Bingwa mtetezi  Faith Kipyegon amewaongoza Wakenya wenza Susan Ejore na Nelly Chepchirchir, kufuzu kwa  nusu fainali ya mbio za mita 1,500 katika michezo ya Olimpiki jijini Paris Ufaransa.

Ejore mwenye  makao yake nchini Marekani alifuzu kwa nusu  fainali,  baada ya kumaliza wa tatu katika mchujo wa kwanza mapema Jumanne akitumia dakika 3 sekunde 59.01.

Kipyegon alifuzu kwa nusu fainali baada ya kumaliza wa nne katika mchujo wa pili kwa muda wa dakika 4 sekunde 00.74.

Chepchirchir aliongoza mchujo wa mwisho wa tatu kwa dakika 4 sekunde 2.67.

Nusu fainali itaandaliwa Agosti nane hulu fainali ikiwa tarehe 10 mwezi huu.

Mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki mwaka 2016 Julius pia amefuzu kwa fainali ya urushaji sagai ,baada ya kuruka umbali wa mita 85.97 yakiwa matokeo yake bora msimu huu.

 

Share This Article