Vipusa wa Kenya wapigwa kikondoo na Korea na kutemwa nje ya Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa akina dada walio chini ya umri wa miaka 17 imebanduliwa kwenye makala ya 8 ya fainali za kombe la Dunia katika Jamhuri ya Dominica, baada ya kupokea kichapo cha mabao matatu bila jawabu kutoka kwa Korea Kaskazini Jumapili usiku.

Mechi ya kundi C ilikuwa ya pili mtawalia kwa Kenya wanaoshiriki kwa mara ya kwanza kupoteza bila hata ya kufunga goli wakisalia wa mwisho bila alama.

Kenya ilikuwa imelazwa mabao 2-0 na Uingereza katika pambano la ufunguzi na watarejea uwanjani kwa mchuano wa mwisho dhidi ya Mexico kabla ya kurejea nchini.

Korea Kaskazini na Uingereza zilifuzu kwa robo fainali baada pia ya Waingereza kupata ushindi wa pili mabao 4-2 dhidi ya Mexico.

Website |  + posts
Share This Article