Vipusa wa Kenya wapigwa dafrau na Wachina huko Uruguay

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba kila upande kwa wanawake – imeanza vibaya msuru wa pili wa mashindano ya raga duniani divisheni ya pili baada ya kucharazwa pointi 19-5 na China Jumamosi jioni mjini Montevideo, Uruguay.

Kenya Lionesses walijipatia try pekee katika mechi hiyo kupitia kwa Edith Nariaka.

Vidosho wa Kenya ambao walizoa alama 12 katika msururu wa kwanza ulioandaliwa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Timu nyingine katika kundi moja na Kenya kwenye msururu wa Uruguay; ni Argentina, Brazil, Afrika Kusini na Uhispania.

Share This Article