Vipers Sports Club ndio mabingwa wa ligi Kuu nchini Uganda msimu wa mwaka 2025/2026.
Klabu hiyo yenye makao yake mjini Kitende, ilihifadhi taji la msimu jana baada ya kuwalemea Maroons FC mabao 3-0 katika uwanja wa Wankulukuku Jumanne wiki hii.
Vipers walitangazwa mabingwa Jumatano jioni baada ya wapinzani wa karibu KCCA kutoka sare tasa na URA FC.
Taji hilo ni la nane la Ligi Kuu kwa Vipers, baada ya kuzoa pointi 64 kutokana na mechi 29.
Vipers SC wanaonolewa na Van Jacky Minnaert, wataiwakilisha Ugandakatika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa mwaka 2025 na 2026.