Viongozi wamwomboleza Rais wa Iran Ebrahim Raeisi

Dismas Otuke
2 Min Read

Viongozi kadhaa wa Ulimwengu wametoa risala za rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raeisi, jumapili jioni baada ya ndege aina ya helikopita  aliyokuwa ameabiri  kuanguka Mashariki mwa Iran.

Viongozi wengi wamemtaja marehemu kuwa  shujaa wa ukombozi na aliyejali utu.

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ametoa risala za rambi rambi akisema alipokea taarifa hizo za tanzania kwa masikitiko makubwa, huku Rais wa Muungano wa Milki za Kiarabu Sheikh Mohammad Zayed, akisema taifa lake linasimama kwa pamoja na Iran wakatihuu mgumu.

Rais wa Urusi Vladmir  Putin ametoa risala za rambi rambi akisema daima atasalia na kumbu kumbu za kiongozi huyo wa kuigwa.

Rais wa Iran Xi Jinping amesema Iran imempoteza kiongozi bora  na rafiki wake wa karibu huku kiongozi wa kundi la mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Seyyed Ali Khamenei akimtaja kuwa mwandani wake wa karibu.

Rais wa Iran Ebrahim Raeisi amatangazwa kufariki kwenye ajali ya ndege iliyotokea Jumapili jioni karibu na milima iliyo kaskazini magharibi mashariki mwa Azerbeijan.

Kiongozi huyo wa Iran alikuwa njiani kurejea ikulu baada ya kufungua bwawa la Qiz Qalasi pamoja na Rais wa Azerbeijan Ilham Aliyev .

Imeripotiwa kuwa ndege aina ya helikopita aliyokuwa akisafiria rais huyo pamoja na Waziri wake wa mambo ya kigeni,Hossein Amir-Abdollahian na maafisa wengine watatu pamoja na marubani, ilianguka kwa kishindo ilipojaribu kutua kutokana na hali mbaya ya hewa .

Miili ya abiria wote waliokuwa kwenye ndege hiyo imepatikana usiku wa kuamkia Jumatatu katika mlim wenye msitu kwenye mabaki ya ndege hiyo.

Mohammad Mokhber ambaye amekuwa makamu Rais wa Raeisi atashikilia wadhfa wa Urais wa nchi hiyo kwa muda.

 

Share This Article