Viongozi wa wanafunzi Bungoma wakutana na mbunge Tim Wanyonyi kujadili mustakabali wa vijana

Francis Ngala
2 Min Read
Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi akiwa kwenye Picha ya Pamoja na Viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kaunti ya Bungoma

Viongozi wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vilivyo Kaunti ya Bungoma wamefanya kikao maalum na Mbunge wa Westlands, Mheshimiwa Tim Wanyonyi, kwa lengo la kujadili masuala yanayowakumba vijana katika taasisi za elimu ya juu.

Katika mazungumzo hayo, Mbunge Tim ambaye pia ametangaza azma ya kuwania kiti cha Ugavana wa kaunti ya Bungoma, aliwahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho vya taifa ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027.

Alisisitiza kuwa ni kwa njia hiyo pekee, vijana wataweza kuwachagua viongozi bora watakaosukuma gurudumu la maendeleo katika kaunti hiyo.

Mbunge huyo pia alionyesha dhamira yake ya kuwa bega kwa bega na vijana, akiwataka kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko chanya nchini. Alieleza kuwa vijana wana nafasi muhimu ya kubadilisha taifa na hawapaswi kuachwa nyuma katika ajenda ya maendeleo.

Kwa upande wao, viongozi hao wa wanafunzi walieleza kuwa mara nyingi vijana wamekuwa wakitumiwa vibaya kisiasa kwa kuwapigia kura viongozi wasiofaa. Hata hivyo, walisisitiza kuwa wakati huu hali imebadilika, na watachagua kwa umakini viongozi wanaowajali na wanaoweka mbele masuala ya maendeleo.

Katika hafla hiyo, vijana waliwahimiza wenzao kujitokeza kwa wingi kuchunguza kwa makini tabia na sera za wagombea kabla ya kufanya uamuzi wa kura, ili kuhakikisha wanachagua viongozi wenye nia ya kweli ya kubadilisha maisha yao.

 

Website |  + posts

I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.