Viongozi wa Nyanza wamkemea Gachagua kwa matamshi yake

Dismas Otuke
1 Min Read

Baadhi ya viongozi wa jamii ya Luo kutoka eneo la Nyanza wamemkemea aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni wakiyataja kuwa yaliyolenga kuleta migawanyiko nchini.

Aidha, wamesema matamshi hayo yalikuwa ya kiholela na yaliyokosa mwelekeo.

Pia wamelaani hatua ya Gachagua kuwatetea viongozi watatu wa serikali waliokamatwa kwa husika kwenye sakata  ya mafuta, wakisema inaashiria kuwa anaunga mkono ufisadi.

Wametaka pia Wakenya kujitokeza kwa wingi na kujisajili kuwa wapiga kura tayari kwa uchaguzi mkuu  wa mwaka ujao.

 

Share This Article