Viongozi wa mashtaka nchini Uhispania wanapendekeza kifungo cha miaka tisa kwa defenda wa Brazil Dani Alves katika kesi ubakaji inayomkabili.
Alves ,aliye na umri 40 wa miaka anadaiwa kumdhulumu kingono mwanamke mmoja katika klabu cha usiku Disemba mwaka uliopita mjini Barcelona.
Tarehe ya kukatwa kwa kesi hiyo haijabainika huku washitaki wakitaka dhamana ya euro milioni 150,000.
Kesi ya ubakaji nchini Uhispania ina adahabu ya kifungo kisichozidi miaka 15 gerezani.
Alves ni mmoja wa wachezaji bora duniani akitwaa mataji 42 yakiwemo matatu ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwa na Barcelona na mawili ya Copa América akiwa na Brazil.