Viongozi wa Kilifi wataka Serikali imkamate mtalii mbakaji

Dismas Otuke
2 Min Read

Viongozi wa kaunti ya Kilifi ameshutumu ongezeko la visa vya ubakaji wasichana wadogo ambayo vimekithiri katika kaunti hiuo na kuitaka serikali kuingilia kati kukomesha uovu huo.

Wakiongozwa na Gavana Gideon Mung’aro viongozi hao wamesema kumwekuwa na ongezeko la visa vya kudhulumiwa kwa wasichana wadgo hususan katika mji wa Malindi wenye shughuli nyingi za kitalii.

Mung’aro amemtaja mtalii mmoja ambaye yamkini amehusika katika visa vingi vya kuwabaka watoto ilihali hachukuliwi adhabu yoyote.

“Visa hivi vingi mnaskia vya ubakaji Kilifii na Mombasa kwa jumla kuna mtalii mmoja ambaye twamjua amedhulumu watoto kadhaa kimapenzi na tutaka serikali imkamate na kumshitaki.”akasema Gavana Mung’aro

Wazizungumza na wanahabari siku ya Jumamosi jijini Nairobi,viongozi hao wameitaka wizara ya mashauri ya Kigeni kuchunguza na kumpokonya mtalii huyo Viza .

Wamewataka akina na mama ambao watoto wao wameathiriwa kuripoti visa hivyo kwa vyombo vya dola na kusaidi kukamamatwa na kushtakiwa kwa mtalii huyo.

“Hatuwezi kuvumilia zaidi ndio maana sisi kama viongozi kutoka Kilifi tumjitokeza kulaani ukatili unaofanyiwa watoto wetu,anawafanyia watoto unyama mwingi na tutatumia kila mbinu hadi atakapomatwa na kushtakiwa,ni starehe gani unayopata ukimdhulumu mtoto sisi tumekataa.”akasema Mbunge Mishi Mboko

Kiongozi wa akina mama kaunti ya Kilifiu Gertrude Mbeyu ana Mbunge wa Kiloni MP Mishi Mboko wamewataka akina kuwa na sauti moja na kusaidia kumaliza uozo huo.

Mbungwa wa kaunti ya Kilifi Gertrude Mbeyu amekashifu ukatili huo akisema “Ni vitendo vya kuogofya na kutamausha na Kando na polisi kumkamata tunataka wizara ya Musalia Mudavadi inayohusika na mambo ya kigeni impokenye viza mtalii huyu .”

Share This Article