Ujumbe wa viongozi wa kidini umekutana na ule wa viongozi wa makundi ya waasi mjini Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ili kujadili kuongezeka kwa hali ya taharuki.
Hii ni baada ya kundi la waasi wa M23 kutwaa mji wa Goma uliopo upande wa mashariki mwa nchi hiyo.
Mkutano huo ulifanyika huku mzozo wa kivita na tatizo la kibinadamu vikiongezeka katika eneo hilo.
Watu zaidi ya 2,000 wamefariki tangu kuanza kwa vita mjini Goma kati ya waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na serikali ya Rwanda dhidi ya wanajeshi wa serikali ya Rais Felix Tshisekedi.
Viongozi hao wa kidini wamesisitiza umuhimu wa majadiliano na kutaka pande zote kusitisha vita.