Viongozi wa Afrika watakiwa kuzingatia ukuaji wa bara hili

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto alihutubia kikao cha pamoja cha Mabunge ya Congo Brazaville.

Rais William Ruto ametoa wito kwa viongozi wa bara Afrika na mabunge yao kutilia mkazo ajenda ya ukuaji wa bara hili.

Rais Ruto aliwarai wabunge nchini humo kuweka sera na sheria zinazohimiza uendelevu wa bara Afrika na kubuni nafasi za ajira kwa raia wake.

Rais amesema bara hili, lina rasilimali za kutosha kutoa nafasi za ukuaji duniani. Haya amesema yatajumwisha uimarishaji wa miundo misingi na kuondoa hitaji la visa ili kuondoa vizingiti vinavyozuia uimarishaji wa biashara.

Aidha, Rais Ruto aliwashauri viongozi kuzingatia mageuzi katika taasisi za fedha duniani, ili kukabiliana tatizo la malimbikizi ya madeni Barani Afrika.

Alidokeza kuwa ni jambo la kujutia kuwa mataifa barani humu yanapaswa kuchagua kati ya mahitaji yao ya maendeleo na hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

“NI bayana kwamba, iwapo hatutashughulikia swala la madeni, itakuwa vigumu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga,”alisema Rais Ruto.

Kiongozi huyo wa Kenya aliyasema siku ya Ijumaa katika kikao cha pamoja cha mabunge ya Congi Jijini Brazzaville, ambako yuko kwenye ziara ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Denis Sassou Nguesso.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *