Vikao vya bunge la Seneti kuanza Jumatatu Turkana

Dismas Otuke
1 Min Read

Vikao vya Bunge la la seneti vitaanza Jumatatu Septemba 25 katika kaunti ya Turkana katika mpango wake maalum wa ‘Seneti Mashinani’.

Ni mara ya kwanza kwa Senati kuandaa vikao vyake katika kaunti hiyo huku vikao vikiendelea hadi tarehe 29 mwezi huu.

Kulingana na sheria bunge la seneti linaruhusiwa kuandaa vikao vyake katika kaunti yoyote nchini kwa mzunguko.

Runinga ya taifa ya KBC Channel 1 na KBC Radio Taifa itapepperusha mbashara vikao hivyo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

TAGGED:
Share This Article