Vijana wa chama cha Orange Democratic Movemen(ODM), tawi la Westlands wamelaani vikali kuvamiwa kwa Mwakilishi wadi wa Kitisuru Alvin Olando.
Vijana hao kutoka eneo bunge la Westlands wakiongozwa na Evans Ochieng,wameshutumu kushambuliwa kwa MCA huyo, wakitaja kuwa hatua ya kinyama inayohujumu demokrasia na sheria za nchi.
Wakiwahutubia wanahabari jana vijana hao walilaalani kushambuliwa kwa MCA huyo katikati ya jiji la Nairobi na kumjeruhi kichwa mkono na mdomo, kabla ya kutibiwa na kuruhusiwa kuondoka katika hospitali ya Aga Khan.
“Sisi kama vijana tunakataa na tunalaani uhuni wa kisiasa na vururugu ambavyo havina nafasi katika nchi yetu,tunataka serikali iwachukulie hatua wahusika wote.”akasema Ochieng
Aidha Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi pia alilaani uvamizi huo akitaja kuwa ukiukaji wa haki za kidemokrasia.