Zaidi ya vijana 500 waliandaa maombi kuwakumbuka wenzao waliofariki wakati wa maandamano ya kitaifa ya vijana wa Gen Z .
Vijana hao walifanya maombi katika bustani ya Jivanjee kaunti ya Nairobi,kabla ya kuelekea katika hospitali kuu ya Kenyatta, kuwatembelea wenzao waliojeruhiwa wakati wa maandamano hayo.