Baadhi ya vijana kaunti ya Kitui wameanzisha mchakato wa kumbandua Gavana wa kaunti hiyo Julius Malombe.
Wakiwahutubia wanahabari mjini Kitui, vijana hao walilalamikia utumizi mbaya wa fedha, ukabila na huduma duni za afya miongoni mwa maswala mengine ambayo yamewashinikiza kuchukua hatua hiyo.
Vijana hao walidai kuwa Gavana huyo amehudumu kama kaimu waziri wa Utalii kwa muda wa miaka miwili, huku katibu wa kaunti hiyo na mkurugenzi wa ukusanyaji ushuru wakikaimu nyadhifa zao katika kipindi hicho.
“Kila kitu kinachofanywa Kitui kinadhibitiwa na familia ya Malombe. Hospitali ziko katika hali duni huku zikizosa vifaa muhimu kama vile dawa,” alisema Augustine Muthiani, mmoja wa vijana hao.
Walitoa wito kwa bunge la kaunti hiyo kukubali ombi lao kumtimua afisini Gavana huyo.