Vifo vya mkasa wa klabu ya usiku huko Dominican vyaongezeka

Paa ya klabu ya usiku ya Jet Set katika jiji kuu la nchi hiyo Santo Domingo iliporomoka.

Marion Bosire
1 Min Read

Idadi ya vifo kutokana na mkasa wa kuporomoka kwa paa ya klabu ya usiku katika Jamhuri ya Dominican vinaendelea kuongezeka na vimefikia zaidi ya 100.

Mkuu wa kituo cha kushughulikia sharura nchini humo Juan Manuel Méndez, alisema kwamba watu 113 walifariki na wengine 155 wakajeruhiwa kwenye kisa hicho katika klabu ya Jet Set.

Mwanamuziki wa mtindo wa Merengue, Rubby Pérez ni mmoja wa waliofariki .

Polisi wanaendeleza oparesheni ya kutafuta na kuokoa manusura huku wakiondoa miili kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo katika jiji kuu la Jamhuri ya Dominica, Santo Domingo.

Tukio hilo la kutisha lilinakiliwa na kamera ambapo video inaonyesha waliokuwepo wakicheza densi wakifurahikia muziki wa Rubby Pérez wakati paa ilianza kuporomoka na kamera zikanakili giza tu baada ya hapo.

Rubby wa umri wa miaka 69 aliondolewa kwenye vifusi kabla ya kuthibitishwa kuwa amefariki muda mfupi baadaye.

Rais wa Jamhuri ya Dominican Luis Abinader alifika katika eneo la tukio ambapo aliombea familia za waathiria na kusema kwamba utawala wake unafuatilia tukio hilo.

Website |  + posts
Share This Article