Makumi ya watu wameuawa na wengine kujeruhiwa katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza kutokana na operesheni zinazoendelea za kijeshi za Israel, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Gaza Adnan Al-Barsh.
Imeripotiwa kuwa watu 10 waliuawa katika mashambulizi mawili tofauti ya anga mapema Jumatatu asubuhi. Mojal ililenga ghorofa katika Mtaa wa Al-Nafaq, kaskazini mwa Jiji la Gaza, na ya pili ililenga nyumba katika kitongoji cha Sheikh Radwan cha jiji hilo. Miongoni mwa waliofariki walikuwa wanawake na watoto kadhaa.
Mwanamke mmoja na mtoto wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio la bomu katika nyumba moja katika kambi ya wakimbizi ya Al-Shati, kaskazini magharibi mwa Gaza City.
Duru za kimatibabu za Palestina zimethibitisha kifo cha mwanahabari Islam Abed, mwandishi Al-Quds Al-Youm, pamoja na mumewe na watoto wake, katika shambulio la anga la Israel lililolenga nyumba ya makazi katika mji wa Gaza Jumapili jioni.