Uwanja wa Kericho Green kuitwa Wilson Chumo Kiprugut

Dismas Otuke
1 Min Read

Uwanja wa Kericho Green utaitwa Wilson Chumo Kiprugut, kwa heshima ya marehemu aliyekuwa Mkenya wa kwanza kushinda medali ya Olimpiki mwaka 1964.

Kiprugut aliyefariki mwaka jana alinyakua medali ya shaba katika mita 800 mjini Tokyo, Japan na baadaye kunyakua nishani ya fedha ya mita 800 mwaka 1968 mjini Mexico .

Uga huo una uwezo wa kumudu mashabiki 10,000 na umetumika kuandaa sherehe za 60 za siku kuu ya  Mashujaa.

Share This Article