Uwanja mpya wa Talanta Sports City kujengwa na vikosi vya KDF

Radio Taifa
1 Min Read

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amekabidhi ujenzi wa uwanja mpya wa Talanta Sports City, ukarabati wa viwanja vya Nyayo, Kasarani na Kipchoge Keino kwa vikosi vya ulinzi nchini.

Hatua hiyo inatarajiwa kupiga jeki maandalizi ya Kenya ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la bara Afrika mwaka 2027 ambapo Kenya pamoja na mataifa ya Tanzania na Uganda wamewasilisha ombi la kuandaa makala hayo.

Namwamba alidokeza kuwa uwanja mpya wa Talanta sports City utakaowaselehi mashabiki elfu 50, unatarajiwa kukamilka katika muda wa miaka miwili.

Katibu katika Wizara ya Michezo Peter Tum alisema kuwa hatua hiyo ni mojawapo ya mikakati inayofanywa na serikali ili kuinua viwango vya michezo nchini.

Katibu katika Wizara ya Ulinzi Patrick Mariru aliahidi kuwa ujenzi na ukarabati wa viwanja hivyo utakamilika jinsi ilivyopangwa na vitajengwa kuambatana na kanuni za shirikisho la soka duniani, FIFA.

Radio Taifa
+ posts
Share This Article