Uvundo wa ufisadi: Ripoti ya EACC yaonyesha Wizara ya Usalama inaongoza

Martin Mwanje
1 Min Read

Wizara ya Usalama wa Kitaifa chini ya uongozi wa Waziri Prof. Kithure Kindiki imeorodeshwa kuwa fisadi zaidi nchini.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde iliyotolewa leo Jumatano na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC juu ya Utafiti wa Maadili ya Kitaifa na Ufisadi 2023.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Wizara ya Afya inayoongozwa na Susan Nakhumicha imeorodheshwa ya pili katika ufisadi huku Wizara ya Uchukuzi ikishikilia nafasi ya tatu.

Wizara za Ulinzi, Elimu na Ardhi zimeorodheshwa katika nafasi za nne, tano na sita mtawalia kati ya wizara ya 22 zilizobuniwa na serikali ya Kenya Kwanza.

Katika hatua inayodhihirisha kuwa Wizara ya Usalama wa Kitaifa ni fisadi zaidi, taasisi zilizo chini ya himaya yake pia zimeorodheshwa kuwa fisadi zaidi.

Katika idara zilizotafitiwa serikalini, Huduma ya Taifa ya Polisi iliorodheshwa kuwa fisadi zaidi ikifuatwa na Idara ya Uhamiaji.  Idara ya Usajili wa Watu imeorodheshwa ya tatu. Idara hizo zote ziko chini ya Wizara ya Usalama wa Kitaifa.

Idara ya afya ya umma imeorodheshwa katika nafasi ya nne miongoni mwa idara fisadi zaidi serikalini ikifuatwa na idara ya elimu katika nafasi ya tano na Tume ya Kitaifa ya Ardhi.

 

Website |  + posts
Share This Article