Utulivu washuhudiwa Meru huku maandamano yakiendelea katika sehemu nyingine nchini

Marion Bosire
1 Min Read

Tofauti na sehemu nyingine za nchi, kaunti ya Meru imesalia tulivu bila maandamano ya aina yoyote ya vijana wa Gen Z.

Badala ya maandamano, baadhi ya vijana wa kaunti ya Meru walitumia fursa hiyo kuridhishwa kwao kuhusu mawaziri aliowateua Rais William Ruto.

Hii ni baada ya jamaa wa umri mdogo kujumuishwa kwenye orodha hiyo ya mawaziri.

Eric Murithi Muga wa umri wa miaka 32 aliteuliwa na Rais kama waziri wa maji na usafi na vijana hao wa Meru wanaonelea kwamba ni hatua nzuri imechukuliwa na Rais katika kuangazia malalamishi ya Gen Z.

TWalimhimiza Rais Ruto aendelee kuteua watu ambao wana uwezo na ujuzi kuhudumu serikalini na wala sio kwa misingi ya kisiasa na kikabila.

Rais ameombwa pia kutafakari kutoa fursa kwa vijana zaidi anapotizamiwa kutoa orodha ya mwisho ya mawaziri.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *