Utoaji chanjo dhidi ya Polio wang’oa nanga kote nchini

Tom Mathinji
1 Min Read
Utoaji wa chanjo dhidi ya Polio wang'oa nanga kote nchini

Serikali za kaunti siku ya Jumamosi zilizindua zoezi la utoaji chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza wa Polio kote nchini.

Katika taarifa, wizara ya afya ilisema zoezi hilo lilianza leo Jumamosi hadi Jumatano tarehe 11 mwezi Oktoba, huku likiwalenga watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano kote nchini.

Katika kaunti ya Nairobi, zoezi hilo lilizinduliwa katika shule ya msingi ya Babadogo.

Wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika kaunti ya Mandera, waziri wa afya wa kaunti hiyo Ali Mohamud, aliwahimiza wakazi kuunga mkono kampeni hiyo, kwa kuwa itasaidia kupunguza maabukizi ya ugonjwa huo katika kaunti hiyo.

Kaunti ya Mandera inalenga kuwachanja watoto 268,678, huku waziri huyo akitoa wito kwa wale wanaotekeleza shughuli hiyo kuhakikisha inafikia asilimi mia moja ya watoto wanaolengwa.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article