Uteuzi wa Phyllis Wagacha kwa tume ya SRC wakataliwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Majengo ya bunge la Kenya.

Kamati ya bunge la Kitaifa kuhusu leba, imekataa uteuzi wa Phyllis Wagacha kuwa mwanachama wa Tume ya Mishahara na Marupurupu, SRC.

Wanachama wa kamati hiyo walisema kuwa umri wa Wagacha tayari umezidi ule wa kustaafu kuambatana na sheria za leba.

Kamati hiyo iliyomsaili Wagacha juma lililopita, iligundua kwamba ana umri wa miaka 75, ambao ni zaidi ya umri wa kustaafu kwa watumishi wa umma licha ya kuwa amehitimu kwa wadhifa huo.

Umri wa kustaafu nchini ni miaka 60.

Hatua hiyo inajiri huku bunge likimuidhinisha Mary Wanyonyi Chebukati kuwa mwenyekiti wa tume ya mapato nchini, KRA.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *