Uteuzi wa mawaziri 19 wapingwa mahakamani

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya Kutetea Haki za Binadamu nchini, KHRC imewasilisha kesi mahakamani kupinga uteuzi wa mawaziri 19 kwa madai kuwa hawakupigwa msasa vyema.

Tume hiyo inataka mahakama kumwagiza Rais William Ruto, kuanzisha upya mchakato wa kuwateua mawaziri kwa kuzingatia katiba.

KHRC pia inadai kuwa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini, EACC ilipuuzwa licha ya kutilia shaka hulka za baadhi ya mawaziri wapya walioteuliwa.

Tume hiyo hususan imehoji ufaafu wa uteuzi wa Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi na ambaye uteuzi wake ulipingwa na EACC.

Pia KHRC inadai maoni yaliyotolewa na Wakenya kabla ya bunge kuwapiga msasaa mawaziri hao hayakuzingatiwa.

Share This Article