Uteuzi wa Charles Githinji katika ubalozi wa DRC wakataliwa

Tom Mathinji
1 Min Read

Hatima ya Charles Githinji,aliyependekezwa na Rais William Ruto kuwa mwakilishi mkuu wa ubalozi wa Kenya Jijini Goma katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, sasa iko mikononi mwa wabunge.

Hayo ni baada ya kamati ya bunge  kuhusu ulinzi na mashauri ya kigeni kuwasilisha ripoti ya kukatalia mbali uteuzi wake.

Kwenye ripoti yake, kamati hiyo ilisema kwamba Githinji hakuoenyesha ufahamu wowote wa majukumu ya wadhifa huo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Nelson Koech alisema waliidhinisha uteuzi wa mabalozi 23 na maafisa wengine wanne wa kibalozi.

Bunge linatarajiwa kujadili ripoti hiyo.

Share This Article