Klabu ya Arsenal ilichukua alama zote tatu nyumbani Emirates baada ya kuwakwaruza mabingwa watetezi wa ligi Manchester City kwa bao moja kwa sufuri.
Mchezo wa Arsenal na Manchester City ulikuwa na mvuto mkubwa kwenye uwanja wa Emirates, vijana wa Mikel Arteta wakitafuta ushindi wa kwanza toka mwaka wa 2015.
Bao la dakika za lala salama la Gabriel Martinelli liliipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao Manchester City katika mechi kubwa zaidi ya msimu huu wa Ligi Kuu ya Uingereza kufikia sasa.
4 substitutes combining for this goal 🥹❤️
Partey→tomiyasu→Havertz→Martinelli https://t.co/4Tk3PxDzSZ
— Selorm (@selormafc) October 9, 2023
Kombora la Mbrazil huyo kunako dakika ya 87 lilimgonga Nathan Ake usoni, na kuelekea kwenye nyavu za City na kuifanya Arsenal kuongoza na kupata pointi tatu muhimu.
Ushindi wa jana dhidi ya Manchester City unaipeleka Arsenal katika nafasi ya pili kwenye jedwali la ligi kuu Uingereza nyuma ya Tottenham Hotspurs ambao wanaongoza kwa alama 20.