Uswizi na Ujerumani zatinga robo fainali ya Euro

Boniface Mutotsi
1 Min Read

Waandalizi wa Euro 2024Ujerumani, wamefuzu kwenye robo fainali ya mashindano hayo baada ya kuwalaza Denmark magoli mawili kwa nunge. Mawili hayo yalipachikwa wavuni na kiungo wa klabu ya Arsenal Kai Havertz kupitia mkwaju wa adhabu kisha kiungo mkabaji wa Real Madrid Jamal Musiala akaongeza la pili namo dakika ya 53 na 68 mtawalia.

Hapo awali, Uswizi iliwabandua mabingwa watetezi Italia kwa mabao mawili bila jibu. Remo Freuler anayehudumu kwa mkopo klabuni Bologna kutoka Nottingham Forest na Ruben Vargas wa klabu ya Augsburg walifunga dakika ya 37 na 46 mtawalia.

Katika robo fainali, Ujerumani itachuana na mshindi wa leo saa nne usiku kati ya Uhispania na Georgia. Uswizi nayo itakabana na bingwa wa leo saa moja siku baina ya Uingereza na Slovakia.

Mechi hizo za robo fainali zitasakatwa tarehe tano na sita saa moja usiku.

Boniface Mutotsi
+ posts
TAGGED:
Share This Article