Uswizi na Ujerumani zafuzu awamu ya pili ya Euro

Marion Bosire
1 Min Read

Mataifa ya Uswizi na wenyeji Ujerumani yameingia kwenye raundi ya timu 16 bora za mashindano ya bara Ulaya. Mataifa hayo yalitoka sare ya goli moja kwa moja katika mtanange wa mwisho wa kundi A ugani Deutsche Bank Park.

Mabao hayo mawili yalipachikwa wavuni kupitia Dan Ndoye na Niclas Füllkrug dakika ya 28 na 90+2 kwa upande wa Uswizi na Ujerumani mtawalia.

Katika uwanja wa MHP, Hungary waliilaza Scotland kwa bao moja lililofungwa kwenye muda wa ziada (90+10) na Kevin Csoboth.

Kufuatia matokeo hayo, Ujerumani imo kileleni mwa kundi hilo kwa alama saba. Uswizi, Hungary na Scotland wanafuata kwa alama tano, tatu na moja mtawalia.

Leo jumatatu saa nne usiku, Uhispania watamaliza dhidi ya Albania wakati Croatia wakifunga na Italia kwenye kundi B.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *