Ushindani kati ya wanamuziki wa kike wa Uganda Cindy Santu na Sheebah Kalunji unaendelea kudhihirika.
Cindy Sanyu ametangaza kwamba ataandaa tamasha lake tarehe ambayo Sheebah alikuwa ametangaza na katika sehemu ile ile ambayo Sheebah alikuwa ametangaza.
Matamasha ya wawili hao yamepangiwa Septemba 15, 2023, katika uwanja mdogo wa ndege wa Kololo.
Tangazo la Cindy limejiri wakati ambapo anamrejelea Sheebah kama mtoto katika tasnia ya muziki na kamwe hawezi kushindana naye.
“Yeye ni mtoto kwango. Nilimwandikia wimbo wake wa kwanza kwa hivyo siwezi kushindana na watoto wangu.” alisema Cindy huku akielezea kwamba yeye ndiye aliandika wimbo “Ngenda Kunyenyeza” wa Sheebah na akampeleka studio kuurkodi.
Anasema mtayarishaji muziki aliyerekodi wimbo huo ni Washington na baada ya hapo akawa anamshika mkono kimziki kwa muda wa mwaka mmoja.
Sheebah hajajibu moja kwa moja tangazo la Cindy la kuandaa tamasha mahali ambapo alikuwa ametangaza na siku ambayo ameichagua.
Lakini alichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa ameshikilia simu na kuandika maneno “Mimi ndio iPhone, wewe ni Nokia” kuonyesha kwamba yeye ni bora kuliko Cindy na ni wa kisasa zaidi.