Mahakama kuu ya Tanzania leo Jumatatu imeanza kusikiliza ushahidi wa serikali katika kesi ya kosa la uhaini dhidi ya mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu.
Ilikuwa mara ya kwanza kwa kesi hiyo kuanza kuskilizwa siku 180, tangu kukamatwa kwa mwanasiasa huyo Aprili 10 mwaka huu.
Katika kesi hiyo Upande wa Jamhuri ulisema utakuwa na Mashahidi takribani 30, huku Upande wa Lissu ukisema utakuwa na mashahidi takribani 15 akiwemo Rais wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakuu wa kiserikali.
Miongoni mwa viongozi wa CHADEMA waliowasili mahakamani ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, John Heche, pamoja na mwanasiasa Godbless Lema.