Usajili wa wanachama wapya wa UDA wazinduliwa Kitui

Marion Bosire
1 Min Read

Viongozi wa chama cha UDA katika kaunti ya Kitui wamezindua mpango wa kusajili wanachama wapya wa chama hicho kwa lengo la kupunguza utawala wa chama cha Wiper katika eneo zima la Ukambani.

Mhandisi Dennis Mwangangi aliyewania wadhifa wa ubunge Kitui Kusini kwa tiketi ya chama hicho alielezea kwamba mpango huo utaanzishwa katika kaunti nyingine ndogo saba za kaunti ya Kitui.

Akizungumza katika ukumbi wa jamii wa Mutomo wakati wa uzinduzi huo, Mwangani alidai kwamba chama cha UDA ni maarufu sana katika kaunti ya Kitui kinyume na dhana ya wengi kwamba eneo hilo limetawaliwa na chama cha Wiper.

Mwangangi aliwasihi wakazi wa Kitui kujitokeza kwa wingi na kujiunga na chama cha UDA ili eneo hilo lipate kufaidi.

Moses Banda, mmoja wa washauri wa Rais William Ruto kwa upande wake aliomba wakenya kuwa na subira na kiongozi wa nchi anaposhughulikia matatizo ya nchi.

Banda alitaja bei ya bidhaa za msingi ambazo alisema zinaendelea kupungua ishara kwamba siku za usoni zitakuwa nzuri nchini Kenya.

Website |  + posts
Share This Article