Upinzani nchini Uturuki kuandamana licha ya marufuku ya serikali

KBC Digital
2 Min Read
Meya wa Istanbul, Ekrem Imamoglu.

yama vya upinzani nchini Uturuki vimewataka wafuasi wao kujitokeza kwa maandamano nje ya bunge mjini Ankara leo licha ya marufuku rasmi ya serikali.

Maandamano hayo yanakuja mwezi mmoja baada ya kukamatwa kwa Meya wa Istanbul, Ekrem Imamoglu — ambaye ni mpinzani mkuu wa kisiasa wa Rais Recep Tayyip Erdogan.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani (CHP) Özgür Özel, ametangaza kuwa atalihutubia taifa nje ya bunge wakati nchi ikiadhimisha Siku ya Uhuru wa Kitaifa (National Sovereignty Day).

Özel aliyechaguliwa kuwa kiongozi wa CHP miezi 18 iliyopita, chama kilichoasisiwa na muasisi wa Jamhuri ya Uturuki, Mustafa Kemal Atatürk — alisisitiza mwito wake wa kuungana kwenye maandamano hayo kupitia chapisho aliloweka kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) Jumanne usiku, licha ya marufuku ya serikali.

“Aprili 23 haiwezi kupigwa marufuku. Mkusanyiko wetu mbele ya bunge na maandamano kuelekea Anıtkabir (kaburi la Atatürk) hayawezi kuzuiwa,” aliandika.

Imamoglu, ambaye pia ndiye mgombea urais wa CHP kwa uchaguzi wa mwaka 2028, alitoa ujumbe kutoka gereza la Silivri mjini Istanbul ambako amekuwa akishikiliwa tangu Machi 23 kwa tuhuma za ufisadi.

“Nitaangalia maandamano haya ya uwakilishi wa kitaifa nikiwa gerezani. Nitakuwa upande wenu, nikitembea pamoja nanyi,” alisema kupitia X.

Kukamatwa kwake kumewasha moto wa maandamano katika miji mikuu ya Uturuki, hasa yakiendeshwa na vijana.

KBC Digital
+ posts
Share This Article