Uongozi wa Jubilee: Kega amtuhumu Kioni kwa kudharau mahakama

Martin Mwanje
1 Min Read

Kaimu Katibu Mkuu wa chama Jubilee Kanini Kega amemtuhumu aliyekuwa mbunge wa Ndaragwa Jeremiah Kioni kwa kuidharau mahakama. 

Chama hicho kimegawanyika mara mbili huku mrengo wa Kega ukiongozwa na mbunge mteule Sabina Chege huku mwingine ukiongozwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.

Kioni ambaye ni Katibu Mkuu wa mrengo unaoongozwa na Rais Mstaafu siku chache zilizopita alidai kuteua wanachama wapya wa Baraza Kuu la Kitaifa, NEC la chama hicho.

Hii ni licha ya mizozo kati ya mirengo hiyo miwili kuwa kiini cha kesi zilizowasilishwa mahakamani na zinazosubiriwa kuamuliwa.

Kega anadai Kioni hana mamlaka ya kutekeleza majukumu aliyojitwika katika siku za hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kuitisha mkutano wowote wa chama na kuteua wanachama wapya wa NEC.

“Timu yetu ya kisheria imeelekezwa kuijuza mahakama kuu yanayoendelea, kuhusiana na namna Kioni anavyoendelea kuidharau na kuweka kando maagizo kuhusiana na uongozi wa chama ili kumwezesha Kioni kuzindua chama chake kipya cha Kamwene,” alisema Kega katika taarifa.

 

 

 

 

Website |  + posts
Share This Article