Uongozi wa AK kusalia afisini kufuatia uamuzi wa mahakama ya rufaa

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama ya rufaa imefutilia mbali uamuzi wa mahakama kuu wa Machi 17 mwaka jana na Jaji Mugambi ulioamrisha waafisa wa kamati kuu ya chama cha Riadha Kenya – AK, kung’atuka afisini.

Mahakama ya rufaa imeitikia ombi la kesi iliyowasilishwa na chama cha Riadha Kenya kupinga uamuzi huo.

Katika uamuzi wa Ijumaa Machi 21, Majaji Pauline Nyamweya, Aggrey Mchelule na George Odunga, wamesema kuwa ombi la kutaka maafisa wote wa AK waondoke afisini haikuwa mojawapo ya mapendekezo ya mlalamishi.

Uamuzi wa mahakama kuu uliwataka viongozi wote wa kamati kuu ya AK, kuondoka afisini, ukisema walikuwa wamehudumu kwa kipindi cha miaka nane wakati kesi hiyo ikiendelea.

Majaji hao walisema uamuzi huo ni kinyume cha sheria za michezo za mwaka 2013.

Uamuzi huo sasa unatoa fursa kwa maafisa wa AK kupanga upya uchaguzi.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mwanariadha mstaafu Moses Tanui miaka tisa iliyopita.

Website |  + posts
Share This Article