Ununuzi wa token za KPLC kusitishwa Jumamosi usiku

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya usambazaji umeme nchini KPLC imetangaza kuwa ununuzi wa umeme kwa njia ya token utasitishwa jumamosi usiku kuanzia saa tano na dakika 50 hadi saa kumi na moja Aljari Jumapili.

Usumbufu huu utapisha ukarabati wa mitambo ya KPLC na wateja wanaotumia huduma ya kununua token za awali au pre paid wametakiwa kununua umeme mapema ili kutoathirika .

Kulingana na taarifa kutoka KPLC wanaonunu tokens kupitia Paybill ya 888880 au Airtel Money hawataweza kununua umeme wa pre paid nyakati hizo.

KPLC huuza umeme kwa njia za pre paid na post paid kwa wateja wake.

TAGGED:
Share This Article