UNGA: Wajumbe waondoka ukumbini Netenyahu akihutubu

Licha ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita - ICC kutoa amri ya kukamatwa kwa Netenyahu  Novemba 21 mwaka 2024, bado kiongozi huyo yuko huru.

Dismas Otuke
1 Min Read

Baadhi ya wajumbe waliondoka nje ya ukumbi wa Kongamano  la 81 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA), wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netenyahu aliposimama kuhutubia kongamano hilo.

Wajumbe hao waliteta kuhusu hatua ya Israel kuvamia Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Nje ya ukumbi jijini New York, hali ilikuwa iyo hiyo huku mamia ya waandamanaji wakikamatwa na polisi.

Waandamanaji hao walibeba mabango yaliyoitaka Marekani imkamate Netenyahu kwa kutekeleza mauaji na ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu.

Licha ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita – ICC kutoa amri ya kukamatwa kwa Netenyahu  Novemba 21 mwaka 2024, bado kiongozi huyo yuko huru.

Hata hivyo, ni vigumu kwa Marekani kumkamata  Netenyahu kwani Israel ni mshirika wa karibu wa nchi hiyo yenye nguvu kubwa zaidi duniani.

 

Share This Article