Umri wa kustaafu kwa watumishi wa umma kupunguzwa hadi miaka 55

Dismas Otuke
1 Min Read

Wabunge wanapendekeza umri wa kustaafu kwa watumishi wa umma upunguzwe kutoka miaka 60 hadi 55.

Kulingana na wabunge hao, hali hii itawapa vijana fursa ya kufanya kazi katika afisi za umma.

Mswada uliowasilishwa bungeni na mbunge wa Embakasi ya Kati Benjamin Gathiru, pia unapendekeza kubuni sheria ambayo haitaruhusu mtu yeyote kuhudumu kama kaimu kwa zaidi ya miezi sita.

Kamati ya leba ya bunge ilijadili mswada huo jana Alhamisi na endapo utapitishwa kuwa sheria, ina maana kuwa watumishi wengi wa umma waliotimiza umri wa miaka 55, watalazimika kwenda nyumbani mapema kwa pamoja hali ambayo pia itaigharimu serikali kiwango kikubwa cha pesa za malipo ya uzeeni.

Umri wa lazima wa kustaafu kwa watumishi wa umma uliongezwa kutoka miaka 55 hadi 60 mwaka 2019.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *