Ukulima wa pareto miaka ya 80 ulikuwa uti wa mgongo kwa wakulima wengi katika kaunti za Elgeyo Marakwet, Nakuru na sehemu nyingi humu nchini.
Hata hivyo, wakulima walikoma kufanya kilimo cha pareto kutokana na kudorora kwa bei na kufungwa kwa kampuni za kununua maua.
Isabella Kiplagat anatokea kijiji cha Koisungur, kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Katika shamba la robo ekari ya pareto, anavuna zaidi ya kilo 20 ya pareto kila baada ya wiki na kuuza kwa shilingi 280 kwa kilo.
Waziri wa Kilimo katika kaunti hiyo Edwin Seronei anasema wanashirikiana na kampuni ya Kentegra kusambaza mbegu na kununua mazao ya pareto kutoka kwa wakulima.