Ukosefu wa usalama wawatia tumbo joto wakazi wa Gem, Siaya

Martin Mwanje
1 Min Read

Wakazi wa eneo bunge la Gem wametoa changamoto kwa asasi za usalama za serikali katika eneo hilo kutoegemea upande wowote wanapofanya uchunguzi kuhusiana na msururu wa hivi punde wa visa vya ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Kulingana na wakazi hao waliojumuisha Mwakilishi wa Wanawake wa kaunti ya Siaya kwenye Bunge la Taifa Dkt. Christine Ombaka na viongozi wa mashinani wa chama cha ODM, kasi ya kobe inayochukuliwa na asasi za usalama kuwachukulia hatua wanaofadhili na kusababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo inatia hofu.

“Katika siku za hivi karibuni tulikuwa na ukosefu wa usalama wakati wa kura za mashinani za ODM ambako makundi yaliyokodiwa yalijaribu kuvuruga uchaguzi huo,” alilalama Dkt. Ombaka.

“Natumai serikali imetilia mkazo hilo kuhakikisha inafanya uchunguzi madhubuti.”

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *