Msanii wa muziki nchini Tanzania Faustina Charles Mfinanga maarufu kama Nandy amemwandikia mume wake William Nicholaus Lyimo maarufu kama Billnass ujumbe wa kuvutia anaposherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
“Hujambo mpenzi ni siku yako, miaka 14 pamoja na ni kama tumeanza jana. Mimi nakupenda bwana! Asante kwa kila kitu asante kwa kuwa kiongozi bora kwangu Mume bora kwangu baba bora kwa Naya shemeji bora kwa ndugu na marafiki zangu mkwe bora kwa wazazi wangu” aliandika.
Aliendelea kwa kumwombea azidi kufanikiwa ili aendelee kuishi maisha mema akisema kwamba tayari ashampa zawadi yake.
“Nakupenda sana Mke Wangu. Katika kitu Mwenyezi Mungu alinipendelea ni Kunipa Wewe na Nafsi itanihukumu nikiacha Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa wewe,” alijibu Billnass.
Nandy na Billnass walifunga ndoa Julai 16, 2022 katika kanisa la KKKT huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam baada ya kuandaa hafla ya kutoa mahari Februari 2022. Wana mtoto mmoja wa kike.
Billnass alizaliwa Aprili 11, 1993 huko Tanga nchini Tanzania na alianza kazi kama mwanamuziki mwaka 2014.