Ujerumani watwaa Kombe la Dunia kwa chipukizi chini ya miaka 17

Dismas Otuke
0 Min Read

Ujerumani wamenyakua Kombe la Dunia kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 17 kwa mara ya kwanza baada ya kuwashinda Ufaransa mabao 6-5 kupitia penalti kufuatia sare ya 2-2 Jumamosi alasiri nchini Indonesia.

Ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kunyakua Kombe la Dunia na wamewatonesha Ufaransa kwa mara ya pili mwaka huu, baada ya kuwashinda kupitia penalti kwenye fainali ya kombe la Ulaya.

Share This Article